Kuanzia tarehe 22 Septemba hadi tarehe 2 Oktoba, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Wang Dinghua ameongoza ujumbe kutembelea Marekani, Kuba na Panama. Amehudhuria kwenye Kongamalo la Wakuu wa Vyuo Vikuu “10+10” vya China na Marekani na kutoa hotuba.
Wajumbe hawa pia wametembelea vyuo vikuu vya Marekani vikiwemo Chuo Kikuu cha Northwestern, Chuo Kikuu cha Chicago, Chuo Kikuu cha Stony Brook cha New York. Pia wametembelea Chuo Kikuu cha Havana cha Kuba, Chuo Kikuu cha Panama pamoja na taasisi yake ya Confucius.
Licha ya hayo, wajumbe hawa wametembelea makao makuu ya Umoja wa Mataifa na Ofisi Kuu ya Shirika la Habari la Xinhua katika Amerika Kaskazini, ubalozi mdogo wa China mjini New York na ubalozi nchini Kuba. Pia wamewatembelea wahitimu wa BFSU wanaosoma na kufanya kazi katika nchi hizo tatu.