Mwanzo > Habari > Content

Makamu Mkuu wa UDSM Atembelea BFSU

Updated: 2024-07-04

Tarehe 1 Julai, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Prof. William Anangisye ametembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Jia Wenjian na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Zhao Gang wamekutana na kuzungumza na mgeni huyo.

Wamezungumzia ushirikiano katika kuendeleza utafiti wa pamoja, mawasiliano ya walimu na wanafunzi, machapisho ya majarida kwa pamoja na pande nyingine.

Wanafunzi wa Kiswahili wamemkaribisha Prof. Anangisye. Baada ya mazungumzo, Prof. Anangisye ametembelea kitivo cha Elimu ya Kimataifa na maktaba ya Chuo.