Mwanzo > Habari > Content

Mkutano wa Umoja wa MOOC ya Lugha za Kigeni wa Vyuo Vikuu vya China Wafanyika BFSU

Updated: 2024-06-26

Tarehe 14 hadi 15 Juni, mkutano wa sita wa Umoja wa MOOC (Massive Open Online Courses) ya Lugha za Kigeni wa Vyuo Vikuu vya China wenye kaulimbiu ya Kuunganisha dunia na kujenga mustakabali kwa teknolojia umefanyika katika Chuo Kikuu cha BFSU.

Mkuu wa Umoja huo Prof. Wang Dinghua ametoa hotuba ya kazi. Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Habari na Mawasiliano cha Idara ya Mawasiliano ya Chama cha CPC Bw. Nong Tao, Mkaguzi wa Idara ya Elimu ya Juu ya Wizara ya Elimu Bw. Song Yi, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Shandong Bw. Cao Xianqiang, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Guangdong Bw. Jiao Fangtai wametoa hotuba kwenye sherehe ya ufunguzi.

Umoja huo pia umefanya kongamano la wakuu wa vyuo vikuu ili kujadili faida ya teknolojia ya kidijitali kwa mageuzi ya elimu ya juu. Pia sherehe ya uzinduzi wa Ushirikiano wa Umoja wa MOOC ya Lugha za Kigeni wa Vyuo Vikuu vya China na Jukwaa la MOOC la Taifa la Thailand imefanyika katika mkutano huo, na makundi bora ya MOOC kwa mwaka huu yametunukiwa tuzo.