HOME > Habari > Content

Kikao cha “Mpango wa Ushirikiano wa Vyuo Vikuu Mia vya China na Afrika” Chafanyika BFSU

Updated: 2024-06-12

Tarehe 31 Mei, kikao cha kutekeleza Mpango wa Ushirikiano wa Vyuo Vikuu Mia vya China na Afrika kimefanyika katika Chuo Kikuu cha BFSU. Mwenyekiti wa Baraza la BFSU na Mkurugenzi wa Mfumo wa Mawasiliano ya Umoja wa Vyuo Vikuu vya China na Afrika Prof. Wang Dinghua, Naibu Mkuu wa Jumuiya ya Elimu ya Juu Bw. Zhang Daliang, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang Bw. Jiang Yunliang wamehudhuria kwenye kikao hicho na kutoa hotuba. Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vyuo Vikuu vya Afrika Prof. Olusola Bandele Oyewole ametoa hotuba kwenye mtandao. Wakilishi wa vyuo vikuu zaidi ya 150 vilivyoshirikishwa katika mpango huo wamehudhuria na kutoa hotuba kuhusu mipango ya kazi.

Mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Ushirikiano wa Ukuzaji wa Wasomi wa China na Afrika uliotolewa na Rais Xi Jinping. Mnamo Agosti, mwaka 2023 Ofisi ya Utendaji wa Mfumo huo ilifunguliwa katika BFSU.