Tarehe 20 Mei, waziri wa elimu Bw. Andrei Ivanets ameongoza ujumbe kutembelea Chuo Kikuu cha BFSU. Mkuu wa BFSU Prof. Jia Wenjian na Naibu Mkuu Prof. Zhao Gang wamekutana na wageni hawa. Pande hizo mbili zimezungumzia kuhusu mawasiliano ya utamaduni na ushirikiano wa elimu. Mkaguzi wa Idara ya Ushirikiano na Mawasiliano ya Kimataifa ya Wizara ya Elimu Bi. Xi Ru pia amehudhuria.
Baada ya mazungumzo, wanafunzi wa Idara ya Kirusi ya BFSU wameghani mashairi ya Belarusi na kucheza ala za jadi za China kwa wageni, ambavyo vimeonyesha matunda ya ujifunzaji ya wanafunzi hao wa Kirusi na Kibelarusi. Wageni hao pia wametembelea Kituo cha Utafiti wa Belarusi cha BFSU. Wamesifia matunda ya kazi za miaka mingi za kituo na kuzungumza na walimu na wanafunzi.