HOME > Habari > Content

BFSU Yaandaa Mazungumzo ya Diplomasia ya Umma kati ya China na Ulaya

Updated: 2024-01-22

Mnamo tarehe 6 Januari, Mazungumzo ya Diplomasia ya umma kati ya China na Ulaya yamefanyika Beijing. Mazungumzo hayo yameandaliwa na Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing na Taasisi ya Taaluma za Utawala wa Kanda na Dunia. Zaidi ya watu 100 kutoka serikali, vyuo vikuu, wataalamu, waandishi wa habari wameshiriki mazungumzo hayo. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan amehudhuria na kutoa hotuba.

Katika mazungumzo hayo, Kituo cha Utafiti wa Umoja wa Ulaya na Maendeleo ya Kikanda cha BFSU kimeanzishwa pia.

BFSU na Jumuiya ya Diplomasia ya Umma ya China pia zimeandaa Kongamano la Diplomasia ya Umma kati ya China na Ulaya lenye kaulimbiu ya Kukuza uelewano, na Kupunguza tofauti.