Mwanzo > Habari > Content

BFSU Yashiriki Mkutano wa Kimataifa wa Lugha ya Kichina

Updated: 2023-12-23

Kuanzia tarehe 7 hadi 9 Desemba, Mkutano wa Kimataifa wa Lugha ya Kichina umefanyika Beijing. Kaulimbiu ya mkutano huo ni Kuhudumia Dunia kwa Kichina, Kufungua Mlango kwa Mustakabali. Zaidi ya wasomi, wataalamu, maafisa wa serikali na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa 2,000 wamehudhuria mkutano huo. Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Wang Dinghua, Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Jia Dezhong na Makamu Mkuu wa Chuo Pro. Jia Wenjian wameshiriki mkutano na kutoa hotuba katika majukwaa maalum.