Kuanzia tarehe 1 hadi 10 Desemba, Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan ameongoza wajumbe kutembelea Ethiopia, Madagaska na Tanzania. Wametembelea Chuo Kikuu cha Addis Ababa, Chuo Kikuu cha Antananarivo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutia saini makubaliano ya ushirikiano baada ya mazungumzo na wakuu wa vyuo husika.
Zaidi ya hayo, Prof. Yang Dan na wajumbe wametembelea makampuni ya China na baadhi ya mashirika ya kimataifa katika nchi hizo kama vile CCECC, CHIEC, Startimes, Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika n.k. ili kuwatafutia wanafunzi nafasi za ajira na mafunzo kwa vitendo.
Ziara hiyo imeimarisha na kupanua wigo wa ushirikiano kati ya BFSU na asasi husika barani Afrika.