HOME > Habari > Content

Wang Dinghua Atembelea Argentina, Brazil na Costa Rica

Updated: 2023-11-24

Kuanzia tarehe 9 hadi 17 Novemba, Mwenyekiti wa Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua ameongoza wajumbe kutembelea Argentina, Brazil na Costa Rica. Wametembelea vyuo vikuu mbalimbali katika nchi hizo na kusaini makubaliano ya ushirikiano ili kuimarisha ushirikiano wa elimu na utafiti, kuongeza ajira kwa wanafunzi na kuchunguza njia mpya ya kuendeleza Taasisi za Confucius. Pia wametembelea Ubalozi wa China nchini Brazil na Costa Rica na kufanya mazungumzo na wafanyakazi wa ubalozi. Katika ziara yake, Prof. Wang Dinghua na msafara wake wamejadiliana na wajumbe wa Shirika la Televisheni la Elimu la China juu ya ushirikiano wa kimataifa wa kusambaza lugha mbalimbali. Pia wamewatembelea walimu na wanafunzi wanaofanya utafiti unaohusu nchi za Amerika Kusini.