HOME > Habari > Content

Mkurugenzi Mkuu wa Zamani wa UNESCO Irina Bokova Atoa Mhadhara katika BFSU

Updated: 2023-11-07

Mnamo tarehe 23 Oktoba, Mkurugenzi Mkuu wa Zamani wa UNESCO Bi. Irina Bokova, ametembelea BFSU na kutoa hotuba yenye mada ya "Utamaduni na Utawala wa Ulimwengu". Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan amehudhuria mhadhara na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Zhao Gang ameendesha mhadhara huo.

Bi. Bokova amefafanua uhusiano uliopo kati ya utamaduni na maendeleo endelevu akielezea uzoefu wa Umoja wa Mataifa katika utekelezaji wa Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu. Pia amejadiliana na wanafunzi kuhusu masuala tofauti yakiwemo “jinsia na maendeleo endelevu”, “utekelezaji wa sheria na mikataba za kimataifa” na “kurudisha urithi wa kiutamaduni”.

Baada ya mhadhara, Prof. Yang Dan amemzawadia Bi. Bokova kitabu cha "Istilahi za Fikra na Utamaduni wa Kichina".