HOME > Habari > Content

Sekretarieti ya Umoja wa Vyuo Vikuu vya China na Afrika yazinduliwa katika BFSU

Updated: 2023-09-15

Tarehe 31 Agosti 2023, Jumuiya ya Elimu ya Juu ya China (CAHE) na Jumuiya ya Vyuo Vikuu vya Afrika (AAU) zimezindua Sekretarieti ya China ya Umoja wa Vyuo Vikuu vya China na Afrika katika BFSU.

Mkuu wa CAHE Bw. Du Yubo, Makamu Mkuu wa CAHE Bw. Zhang Daliang, Katibu Mkuu wa AAU Prof. Olusola Oyewole na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua wamehudhuria sherehe ya uzinduzi huo.

Chini ya mwongozo wa Wizara ya Elimu na Jumuiya ya Elimu ya Juu ya China, Sekretarieti ya China ya Umoja wa Vyuo Vikuu vya China na Afrika itashirikiana kwa kina na vyuo vikuu na taasisi za utafiti za Afrika nchini China, na kujenga mtandao wa ushirikiano wa utafiti wa kitaaluma kati ya China na Afrika.