HOME > Habari > Content

Karibuni Wanafunzi Wapya wa 2023

Updated: 2023-09-15

Mnamo Septemba 4, sherehe ya kuwakaribisha wanafunzi wapya wa 2023 imefanyika hapa Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing. Kwa ujumla, wanafunzi wapya 3,267 wamejiunga na chuo hiki na kuanza maisha mapya.

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua, Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan na aliyekuwa Naibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano ya Kimataifa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Ai Ping wamehudhuria sherehe hiyo.

Prof. Yang Dan ametoa hotuba ya kuwakaribisheni wanafunzi wapya kwa dhati. Prof. Wang Dinghua amewavalia wawakilishi wa wanafunzi nembo za chuo kikuu na kuwapa kadi za chuo.