Mwanzo > Habari > Content

Kongamano la Ustaarabu wa Ulimwengu Lafanyika BFSU

Updated: 2023-09-20

Mnamo Septemba 16, Kongamano la Ustaarabu wa Ulimwengu limefanyika katika Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing. Kaulimbiu ya kongamano ilikuwa “Kuwasiliana na Utamaduni wa Ulimwengu ili Kuongeza Uelewa wa Kimataifa”. Zaidi ya watu 600 kutoka serikalini, vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi, wataalamu, wanafunzi na walimu wa BFSU wameshiriki kongamano hilo. Kongamano hili linakusudia kusherehekea miaka kumi ya mkakati wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua amefanya hotuba yenye mada ya “Kuonyesha majukumu ya chuo kikuu katika utekelezaji wa ustaarabu wa ulimwengu”. Naibu Waziri wa Idara ya Uhusiano wa Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Guo Yezhou, aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Irina Bokova na viongozi wengine pia wametoa hotuba.

Katika Kongamano hilo, matokeo ya elimu ya utamaduni ya mataifa ya “Ukanda Mmoja, Njia Moja” yametolewa, jukwaa la huduma ya lugha ya kimataifa limezinduliwa rasmi, na fahirisi ya mchango wa uelewa wa kimataifa imetangazwa.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan ametoa hotuba ya “Kukuza mawasiliano ya ustaarabu ili kuongeza uelewa wa kimataifa”. Wataalamu na viongozi wengine pia wametoa hotuba zilizozingatia namna ya kuimarisha mawasiliano na maingiliano ya kimataifa.

Mada za majukwaa sambamba ni “Jumuiya yenye Mustakabali wa Pamoja: Changamoto na Mustakabali”, “Lugha na Ustaarabu wa Binadamu”, “Usawa wa Elimu na Mustakabali wa Dunia” na kadhalika. Wasomi na wataalamu wa ndani na nje ya nchi wamejadiliana kwa kina juu ya mada hizo.