Mnamo tarehe 22 Septemba, Kongamano la Mawasiliano ya Kimataifa ya Utamaduni wa China limefanyika Beijing. Kongamano hilo liliandaliwa na Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing, Shirika la Uchapishaji wa Kimataifa la China na Taasisi ya Utamaduni wa China.
Mada ya kongamano hili ni “Tekeleza Mipango ya Ustaarabu wa Kimataifa na Kukuza Maendeleo ya Ustaarabu wa Binadamu kwa Pamoja ”. Takriban wataalamu 400 wa ndani na nje ya China kutoka nyanja mbalimbali wameshiriki kongamano hilo. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan amehudhuria sherehe ya ufunguzi na kutoa hotuba.