Mnamo tarehe 26 Septemba, Mke wa Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Syria Bi. Asma al-Assad ametembelea BFSU na kutoa hotuba kwenye Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Kitivo cha Kiarabu. Pia amekutana na wawakilishi 40 kutoka balozi, vyuo vikuu na taasisi za utafiti. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Jia Wenjian amehudhuria hafla hiyo na kutoa risala.