Tarehe 4-5 Desemba, Mkutano wa 13 wa Taasisi za Confucius Duniani umefunguliwa na Naibu Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Makao Makuu ya Taasisi za Confucius Bi. Sun Chunlan mjini Chengdu. Kaulimbiu ya mkutano huo ni “Kukua kwa mageuzi na ubunifu, Kujenga mustakabali kwa ushirikiano”. Wajumbe zaidi ya 1,500 kutoka nchi 154 wamehudhuria mkutano huo wakiwamo Mkuu wa chuo Prof. Peng Long na makamu mkuu Prof. Yan Guohua.
Kwenye mkutano huo, chuo chetu kimepewa tuzo ya “Mshirika Bora wa Taasisi za Confucius” kwa mara ya nne. Taasisi ya Confucius ya Barcelona (CIAB), Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Rome La Sapienza (CIURLS) na Taasisi ya Confucius ya Nürnberg-Erlangen (CIN) zinazoendeshwa na chuo chetu zimetunukiwa tuzo ya “Taasisi Bora ya Confucius” mwaka huu.