Mkuu wa Chuo Kikuu Prof. Peng Long amefanya ziara nchini Panama, Ecuador na Argentina kuanzia tarehe 13 hadi 21 Septemba.
Katika ziara yake, Prof. Peng amevizuru Chuo Kikuu cha Panama, Chuo Kikuu cha Cuenca na Chuo Kikuu cha Ecuador, Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Argentina, Chuo Kikuu cha Buenos Aires, Chuo Kikuu cha Córdoba na Chuo Kikuu cha UADE na kuzungumza na wakuu wa vyuo hivyo. Pia amekutana na mabalozi wa China katika Panama na Ecuador.