HOME > Habari > Content

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Lugha cha Munich Azuru BFSU

Updated: 2019-04-28

Novemba 16 asubuhi, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Lugha cha Munich (SDI) Bw. Felix Mayer amezuru chuo chetu na kutunukiwa cheti cha profesa mwalikwa.

Mkuu wa Chuo Prof. Peng Long amekutana na mgeni huyu akisema ushirikiano baina ya vyuo viwili katika mradi wa wakalimani wa shahada ya uzamili umetupa moyo wa kuzidisha ushirikiano katika sayansi ya siasa, uchumi, mahusiano ya kimataifa na nyinginezo licha ya fani za ukalimani na utafiti wa Ujerumani.

Bw. Felix Mayer ameshukuru kupewa nafasi ya kutoa mhadhara wa matumizi ya teknolojia katika fani ya ukalimani. Yeye pia anatarajia ushirikiano wa pande mbili upanuke zaidi katika mawasiliano ya walimu na wanafunzi, utafiti wa ufundishaji na taasisi ya Confucius.