HOME > Habari > Content

Naibu Waziri wa Elimu wa Syria Azuru BFSU

Updated: 2019-04-28

Tarehe 25 Novemba, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Prof. Wang Dinghua amekutana na Naibu Waziri wa elimu wa Syria Bw. Farah Sulaiman Al. Mutlak.

Profesa Wang amewaelezea wageni historia ya chuo na maendeleo ya taaluma ya Kiarabu. Anatarajia chuo chetu na vyuo vikuu vya Syria vishirikiane zaidi katika ufundishaji na utafiti wa lugha ya Kiarabu.

Bw. Al. Mutlak amesema Syria ina idadi kubwa ya walimu wa Kiarabu ambao watahakikisha ushirikiano wa pande mbili. Kwa kuchukua nafasi hii, yeye pia ameonesha furaha ya kualikwa katika Kongamano la Pili la “Elimu ya Nchi za Ukanda mmoja na Njia moja” na kuzungumza na wadau wa duniani.

Kongamano hili lililoandaliwa na chuo chetu limehudhuriwa na wataalamu zaidi ya 50 kutoka nchi tisa. Wataalamu hao watazungumzia “Raslimali, Ukuaji wa Uchumi na Maendeleo ya Taifa”, “Utamaduni wa Elimu ya Kitamaifa”, “Utandawazi, Uzalendo na Usasa” na “Uchunguzi, Uvumbuzi na Maendeleo Endelevu”.