Mwanzo > Habari > Content

Kambi ya Majira ya Joto ya Daraja la Kichina ya 2021 yafanyika BFSU

Updated: 2021-08-16

Kuanzia tarehe 20 Julai hadi tarehe 7 Agosti, BFSU imefanya miradi kadhaa ya mawasiliano ya Daraja la Kichina la mwaka 2021 kupitia mtandao ikiwa in pamoja na Kambi ya Majira ya Joto ya "Immersion na Impression" mtandaoni kwa wanafunzi wa sekondari wa Ulaya, Kambi ya Majira ya Joto kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na kadhalika.

Miradi ya mawasiliano ya Daraja la Kichina ya 2021 inajumuisha ujifunzaji wa lugha katika madarasa madogo, mihadhara ya kitamaduni katika madarasa makubwa, na kurusha matangazo ya moja kwa moja na video zilizorekodiwa ili kuwasaidia wanafunzi kufahamu China kwa undani na kutumia lugha ya Kichina kwa ufanisi zaidi.

Kambi ya Majira ya Joto ya “Immersion na Impression” na Kambi ya Majira ya Joto kwa wanafunzi wa vyuo vikuu zinajumuisha mitalaa ya lugha ya Kichina, tamasha la utamaduni wa kijadi wa China, mihadhara inayohusu China na video mbalimbali. Wanafunzi 176 wanaotoka nchi 11 zikiwemo Urusi, Hungary, Bulgaria, Jamhuri ya Czech, Uhispania na kadhalika wameshiriki kwenye kambi hizo.

Kambi ya Majira ya Joto ya "Kutafuta China—kitovu cha Lingnan" inayozingatia urithi na maendeleo ya historia na utamaduni wa eneo la Lingnan Imewavutia wanafunzi 97 kutoka nchi 14 zikiwemo Ujerumani, Luxemburg, Ureno, Uingereza na Poland kushiriki.