Mwanzo > Habari > Content

Karibuni Wanafunzi Wapya wa 2021

Updated: 2021-09-09

Mnamo Septemba 7, sherehe ya kuwakaribisha wanafunzi wapya wa 2021 ilifanyika hapa Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing. Kwa ujumla, wanafunzi 3,400 wapya wamejiunga na chuo hiki na kuanza maisha yao mapya. Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Wu Hongbo, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua, Mkuu wa Chuo Kikuu Prof. Yang Dan, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Zhao Gang na viongozi wengine walihudhuria sherehe hiyo. Yang Dan aliwapongeza wanafunzi na kuwakaribisheni kwa dhati.