Tarehe 23 Oktoba, Kongamano la pili la Elimu Linganishi na Elimu ya Kimataifa limefanyika mjini Beijing.
Katibu Mkuu wa Tume ya Kitaifa ya UNESCO Bw. Qin Changwei na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua walihudhuria kongamano hilo.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua ametoa hotuba ya “Kuimarisha Ushiriki wa China katika Usimamzi wa Elimu ya Dunia”. Ameweka wazi mambo matano muhimu ya kufanya: 1) kutayarisha wasomi wa usimamizi wa elimu ya dunia; 2) kutafiti usimamizi wa elimu ya dunia; 3) kuimarisha uwezo wa kuieleza China kwa undani; 4) kuzidisha ushirikiano na taasisi za kimataifa; 5) kujenga jukwaa la ushirikiano la kimataifa.
Programu za Taasisi ya Elimu ya Maldives na Nepal Resources Himalaya Foundation zimetunukiwa Tuzo ya Wenhui ya Ubunifu wa Elimu katika Kanda ya Asia-Pasifiki kwenye kongamano hilo.