Tarehe 19 Oktoba, Tamasha la Sita la Vijana wa China na Afrika limefanyika mjini Beijing. Vijana 45 wanaotoka nchi 44 za Afrika na wanafunzi 38 wa BFSU wamealikwa kushiriki kwenye tamasha hilo.

Mwenyekiti wa Mfuko wa Song Qingling wa China Bw. Wang Jiarui, Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje Bw. Deng Li na Balozi wa Nigeria nchini China Bw.Baba Ahmad Jidda wametoa hotuba katika ufunguzi wa tamasha hilo. Vijana wa China na Afrika wametoa hotuba pia wakielezea nia imara ya kuchangia pakubwa zaidi katika ushirikiano kati ya China na Afrika.
Baada ya ufunguzi, wanafunzi wa BFSU pamoja na wenzao wa Afrika walijifunza elimu ya utamaduni wa kijadi wa China wakizidisha maelewano kwa ushiriki wa pamoja.

Mkuu wa Kitivo cha Masomo ya Afrika Prof. Li Hongfeng ametoa hotuba ya “Ushiriki wa pamoja wa vijana wa China na Afrika katika kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye hatma ya pamoja” katika kongamano la pili, alisisitiza kuwa haki na kuheshimiana ni jiwe la msingi la ushirikiano kati ya China na Afrika.

Wanafunzi wa BFSU wamehutubia kongamano la “Nafasi ya Vyama vya Siasa katika Maendeleo ya Taifa” wakielezea umuhimu wa vijana katika maendeleo ya China na Afrika ya siku za usoni.