Mnamo Novemba 10, mafunzo ya watu wanaojitolea wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Mwaka 2022 yamezinduliwa katika BFSU. Walimu na wanafunzi wanaojitolea wa BFSU karibu 500 wameshiriki kwenye uzinduzi huo.
Mafunzo hayo yatakayoendelea kwa mwezi mmoja yataboresha uwezo na stadi za wanafunzi wanaojitolea wa BFSU kwa kiasi kikubwa.
BFSU itatuma zaidi ya wanafunzi wanaojitolea 800 wakati Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu itakapofanyika. Wanafunzi hao watatoa huduma za lugha, mapokezi, NCS, OFS, maonyesho ya michezo na uendeshaji wa vyombo vya habari. Aidha, karibu walimu na wanafunzi 100 watatoa huduma ya tafsiri katika Kituo cha Huduma za Lugha mbalimbali cha Beijing.