Mwanzo > Habari > Content

Kongamano la Wasomi wa Ndani na Nje ya Nchi wa Taasisi za Confucius za BFSU la 2021 lafanyika

Updated: 2021-12-12

Tarehe 9 Desemba, Kongamano la Wasomi wa Ndani na Nje ya Nchi wa Taasisi za Confucius za BFSU la 2021 limefanyika. Kongamano hilo lenye kaulimbiu ya "Elimu ya Lugha ya Kichina Duniani Baada ya Janga la UVIKO-19" linalenga kutatua matatizo yanayoikabili elimu ya lugha ya kichina katika siku za usoni, kujadili jinsi ya kubadilisha changamoto kuwa fursa, na kusukuma mbele maendeleo ya elimu ya lugha ya Kichina duniani.

Mkuu wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua, Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Korea ya Kusini Prof. Kim In-Chul na wageni waalikwa wamehudhuria ufunguzi wa kongamano. Wawakilishi wa taasisi za Confucius wamefanya majadiliano juu ya mada mbili. Takriban watu mia moja wameshiriki kwenye kongamano hilo.