Mwanzo > Habari > Content

Wanafunzi wanaojitolea wa BFSU wako tayari kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya 2022

Updated: 2022-01-22

Mnamo 18 Januari, BFSU imeandaa sherehe ya kuwasindikiza wanafunzi wanaojitolea wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Mwaka 2022. Naibu Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi Bw. Wan Xuejun, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua, Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof.Yang Dan na viongozi wengine wamehudhuria sherehe hiyo.

BFSU itatuma zaidi ya wanafunzi wanaojitolea 900 kuihudumia Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu wakati itakapofanyika. Kwa niaba ya BFSU, Prof. Wang Dinghua ameikabidhi bendera ya Timu ya Kujitolea ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi kwa wanafunzi ikiashiria kuwa wanafunzi wanaojitolea wa BFSU wapo tayari kwa kazi hiyo.

Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi inakaribia, na Kituo cha Huduma za Lugha Mbalimbali cha Beijing kitatoa huduma za ukalimani katika lugha 21 kwa Michezo hiyo.

Bw. Wan Xuejun ametoa shukrani kwa wanafunzi na walimu wote wa BFSU wanaotoa huduma katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi akiwataka watekeleze majukumu yao na kufanya kazi kwa kadri wawezavyo. Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Dr. Su Dapeng ametoa matumaini yake na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Dr. Ding Hao amekabidhi vifaa kwa wanafunzi wanaojitolea.