Feb.6 Tianshan News/Xinjiang Leo, Urumqi. Majira ya saa 10 kasorobo mchana, Februari 5, Dinigeer Yilamujiang na mwenzake Bayani Jalin wameonekana kwenye mbuga ya kuteleza kwenye theluji. Hii ni mara ya kwanza ya kuwakuta wachezaji wanaotoka wilaya ya Altay ya mkoa wa Xinjiang ambapo ni chimbuko la utelezaji theluji wa binadamu katika historia ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi.
Usiku wa Februari 4, Dinigeer aliwasha mwenge mkuu wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi katika Uwanja wa Taifa akiwa anatarajia kutimiza ndoto ya baba yake.
Baba yake alikuwa mchezaji wa kuteleza juu ya theluji kwenye mbuga. Msichana huyu mwenye umri wa miaka 20 mwaka huu amemfuata baba yake kuteleza juu ya theluji tangu alipokuwa na umri wa miaka minane. Baba yake Dinigeer amesisimuka sana akisema kuwa, “Nimefurahi sana hata siwezi kutamka neno maana binti yangu leo ametimiza ndoto yangu.”
Dinigeer alizaliwa katika wilaya ya Altay iliyopo kaskazini-magharibi mwa China. Huko kwenye pango moja la Dunde Bulak kuna mchoro wa rangi juu ya mwamba ambao umeonyesha watu wa kale walivyowinda kwa kuteleza juu ya theluji. Wataalamu wamethibitisha kuwa mchoro huu una historia zaidi ya miaka 12,000 na ni kumbukumbu ya zamani kabisa ya binadamu ya kuteleza kwenye theluji.