Mwanzo > Habari > Content

Gu Ailing: Nina Jukumu la Kuwafahamisha Vijana wa China Utelezaji Theluji wa Freestyle

Updated: 2022-02-09

BEIJING. Februari 7, Mchezaji wa China Gu Ailing (Eileen) ameonekana katika jukwaa la utelezaji theluji wa freestyle akiwa amevaa vazi lenye mchoro wa joka la dhahabu. Jukwaa hilo limejengwa kwenye mahali ambapo palikuwa Kiwanda cha Chuma na Chuma cha Pua cha Beijing.

Msichana huyu mwenye umri wa miaka 18 ameanza kuiwakilisha China-nchi ya asili kwa upande wa mama-kushiriki mashindano ya kimataifa tangu mwaka 2019 akikusudia kuongeza umaarufu wa michezo hiyo nchini China hasa miongoni mwa vijana. Katika mahojiano amesema, “Sidhani kuwa ni watu wazima tu wana sauti na ushawishi kwa shughuli za kimataifa. Sasa wakati umefika kwa sisi vijana kutoa sauti yetu na kuleta mabadiliko katika masuala yanayotuhusu.”

Sasa hivi zaidi ya watu milioni 300 wamejiunga na michezo ya majira ya baridi nchini China. Gu amesema lengo lake ndio kuwashirikisha watu wengi zaidi katika mchezo wa kuteleza juu ya theluji kwa freestyle na kuwaonesha furaha za michezo, japo nafasi yake ni ndogo lakini amefurahi pia.

Katika mahojiano alituonyesha mchoro wa joka la dhahabu uliochorwa kwenye vazi lake. Alisema mchoro huu wa kichina ulibuniwa na yeye mwenyewe.