BEIJING. Februari 9, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanywa na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) na Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, Bw. Li Sen, mkurugenzi wa idara ya mipango, ameeleza hatua za kuchukuliwa kwa kuandaa “Michezo ya Olimpiki ya Kijani” akitumia dhana za “usimamizi wa kaboni za chini” na “hifadhi ya mazingira”.
Safari hii Beijing imetumia majumba sita ya Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008. Nishati za umeme zilizozalishwa katika Zhangjiakou zimesafirishwa hadi maeneo matatu ya michezo yaani Beijing, Yanqing na Zhangjiakou kupitia “Njia Kuu ya Umeme wa Kijani” ili kuhakikisha matumizi ya umeme kuwa ya kijani yafikie asilimia 100. “Kwa jumla, katika miaka sita ya maandalizi iliyopita, tumetimiza ufyonzaji wa hewa ya ukaa kwa kupunguza utoaji wa hewa ya kaboni kwa kiasi kikubwa na kuweka utaratibu wa kulipa fidia na kutoa michango kwa makampuni,” amesema Bw. Li Sen.
Eneo la mashindano la Yanqing ni mojawapo ya maeneo ya michezo ya theluji, ambapo kuna rasilimali nyingi za kimaumbile. Kamati ya Maandalizi imetumia njia tofauti za kuhifadhi mimea kulingana na masharti ya ukuaji wa mimea tofauti. Aidha, Kamati ya Maandalizi imefanikiwa kuondoa udongo wa juu jumla ya mita za ujazo 81,000 na kufanya ufufuaji wa kiikolojia. Na udongo wote ulioondolewa umetumika kwa ufufuaji wa kiikolojia na ujenzi wa mandhari ndani ya eneo la mashindano.