Mwanzo > Habari > Content

Kadi Nzuri ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi

Updated: 2022-02-12

Februari 10 ni siku ya kwanza ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China. Gao Xiaofan alipomaliza kazi yake ilikuwa saa kumi na mbili alfajiri. Siku hiyo ni siku yake ya kuzaliwa pia, lakini haikuwa tofauti na siku nyingine tangu alipokuwa msaidizi wa Ujumbe wa Ukraine kama mtu anayejitolea kutoka Chuo Kikuu cha BFSU. Yeye ni mmojawapo wa wanafunzi wanaojitolea 900 kutoka chuo hiki.

“Hapa kila mtu ni sawa na anaheshimiwa. Sisi tunafanya kazi kwa bidii kwa ajili ya lengo moja. Hakuna madaraja. Hayo ndiyo mazingira mazuri ya kazi niliyotarajia,” alisema Che Jiayi ambaye ni msaidizi wa Ujumbe wa Marekani. Zou Guanglin, msaidizi wa ujumbe wa Japani, alimkubali vile vile. Wanacheka pamoja, wanatazama michezo pamoja, wanafanya kazi pamoja. Hayo yote yalimuelewesha Guanglin maana ya “timu”.

Kwa wanafunzi hawa wanaojitolea, hii siyo ni fursa ya kazi tu, lakini pia ni fursa ya kujiinua. Kila mtu amepata maendeleo makubwa katika mwezi mmoja uliopita, na kila mgeni wanayempokea ni mwalimu na rafiki yao mzuri.

Tarehe 31 Januari ni mkesha wa mwaka mpya wa jadi ambao wananchi wa China hujumuika na wanafamilia yao kwa jadi ya kichina. Lakini mwaka huu wanafunzi hawa walipitisha siku hiyo kazini. “Katika basi lililokwenda uwanjani, mchezaji mmoja aliniambia, ‘Inasikitisha kuwa huwezi kuwa pamoja na familia yako, lakini naamini wanakuonea fahari.’” Jiayi alifarijika baada ya kusikia hiyvo.

Saa mbili usiku mnamo tarehe 4 Februari, sherehe ya ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ilipoanza, wanafunzi walikuwa wanashughulikia kuwakaribisha wajumbe na kuwaongoza kukaa kwenye viti vyao. “Ninapitia historia, na mimi nimekuwa sehemu ya historia,” Zou Guanglin alisema.

Kila siku kwenye basi la kuelekea Kijiji cha Olimpiki, Gao Xiaofan anapenda kukaa karibu na madirisha kuona jua likichomoza na rangi ya mbingu ikibadilika kuwa rangi ya dhahabu. Kila siku wana shughuli nyingi na hawana muda wa kupumzika. Hii imekuwa kawaida ya kazi yao.