Feb.18, 2022, Beijing. Shannon Abeda mwenye umri wa miaka 25 ni mchezaji wa kuteleza theluji kwenye mlima kutoka Afrika katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing. Naye pia ni mmojawapo kati ya wachezaji 6 wa bara la Afrika kwenye michezo hiyo. Amemaliza mashindano yake kwa nafasi ya 39 ambayo haina nafasi ya kutwaa medali, lakini ameinua nafasi yake zaidi ya 20 kuliko nafasi ile katika Michezo ya Olimpiki ya Pyeongchang.
Huyo “mchezaji bora wa Afrika” anatoka Eritrea, nchi ambayo iko pembe ya bara la Afrika. Shannon Abeda alionekana katika jukwaa la Olimpiki kwa mara ya kwanza mwaka 2018 huko Pyeongchang. Baadaye aliwahi kustaafu kwa sababu ya majeraha na magonjwa yake. Lakini kifo cha ghafla cha rafiki yake kilimfanya kijana huyo aangalie maisha yake na masikitiko ya maishani tena. Mnamo Novemba 2020, Shannon Abeba alirudia katika mchezo huo akiwa anatamani Waafrika wengi zaidi washiriki kwenye michezo ya majira ya baridi kupitia Michezo ya Olimpiki ya Beijing.
“Natumai mfano wangu uwaondolee watu wa rangi vikwazo vyote vya kushiriki katika michezo hiyo. Sitaki wana hofu ya kujaribu,” Abeda alisema. Hadithi yake imewapa watu moyo, na wachezaji wa Afrika wameanza kuwasiliana naye wakitamani kuanzisha chama cha michezo ya kuteleza kwenye theluji ili wachezaji wa Afrika wajumuike pamoja na kuwavutia watu wengi zaidi.