Kuanzia Machi 19 hadi 20, Kongamano la 6 la Kitaifa la Mageuzi na Maendeleo ya Elimu ya Lugha za Kigeni katika Vyuo Vikuu limefanyika katika FLTRP. Kaulimbiu ya kongamano hilo ni "Kuielewa China, Kuunganisha Dunia".
Naibu Mkurugenzi wa Ofisi ya Mawasiliano ya Kimataifa ya Idara ya Uenezi ya CPC, Bw. Chen Xueliang, Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya Juu ya Wizara ya Elimu, Bw.Wu Shixing, Balozi wa zamani wa China nchini Uingereza, Bw. Zha Peixin na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua wametoa hotuba za mada husika.
Prof. Wang Dinghua amedhihirisha njia kumi zinazoviwezesha vyuo vikuu vya China kushiriki katika uongozi wa kimataifa.
Kongamano hilo limefungua majukwaa tisa ya mada tofauti, na wadau 92 wamezungumzia masuala ya elimu ya lugha za kigeni na kujadili muundo mpya na maendeleo mapya ya lugha za kigeni ya China.
