Mnamo Aprili 1, mkutano wa nane wa Chama cha Tafsiri na Ukalimani cha China (TAC) umefanyika Beijing. Naibu Katibu Mkuu wa Idara ya Uenezi ya CPC Bw. Lv Yansong, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kimataifa ya Watafsiri Bw. Kevin Quarkna viongozi wengine wametoa hotuba katika hafla ya ufunguzi. Baraza jipya la uongozi limechaguliwa, na makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Sun Youzhong amechaguliwa kuwa naibu mkuu wa baraza hilo.
Mkutano huo umetoa tuzo mbalimbali kwa watafsiri hodari. Maprofesa saba wa BFSU wametunukiwa heshima ya “Watafsiri Wazoefu”. BFSU imepewa heshima ya “Mwanachama Bora” na Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani kimepewa heshima ya “Idara Bora” kutokana na mchango mkubwa katika Kupambana na Janga la Korona.