Mwanzo > Habari > Content

Kazi za kujitolea za BFSU katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi Zasifiwa

Updated: 2022-04-25


Tarehe 19 Aprili, mkutano wa kutoa tuzo kwa kazi za Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu umefanyika katika Jumba la Makumbusho la Shougang.

Timu ya wanaojitolea ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya BFSU na Kituo cha Huduma za Lugha Mbalimbali cha Beijing zimepata tuzo ya “Kundi Bora katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu”. Wanaojitolea wa BFSU Liu Zhipeng na Ye Wenxiaoyu wametunukiwa tuzo ya “Mtu Bora Anayejitolea katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu”. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof.Yang Dan na wawakilishi 20 wa wanafunzi wanaojitoleai wamehudhuria mkutano huo.

BFSU ilituma wanaojitolea 900 katika kumbi 13 za michezo wakati Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ilipofanyika. BFSU ndiyo chuo kikuu kinachoongoza kwa idadi ya wanaojitolea wa kitaaluma. Aidha, BFSU ilijenga Kituo cha Huduma za Lugha Mbalimbali cha Beijing ambacho kilikidhi mahitaji ya lugha ya wajumbe na watu wengine walioshiriki katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu.