Mwanzo > Habari > Content

Jumuiya ya Utafiti wa Maeneo ya Kimataifa (CCAS) Yazinduliwa BFSU

Updated: 2022-05-09


Mnamo Aprili 29, 2022, uzinduzi wa Jumuiya ya Utafiti wa Maeneo ya Kimataifa(CCAS) umefanyika katika BFSU.

Jumuiya ya Utafiti wa Maeneo ya Kimataifa imeanzishwa na Muungano wa Vyuo Vikuu vya Lugha za Kigeni vya Duniani(GAFSU), ambayo ni mtandao wa kitaaluma unaojumuisha wasomi wa lugha zaidi ya 100 kutoka nchi 181.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan ametoa hotuba ya ukaribisho na kueleza matarajio yake juu ya uanzishwaji wa Jumuiya ya Utafiti wa Maeneo ya Kimataifa kutoka pande tatu: Kwanza ni kukabiliana na changamoto za kimataifa na kuchangamkia fursa kwa pamoja kupitia ushirikiano; Pili ni kuhimiza ushirikiano wa wasomi wanaoshughulikia utafiti wa maeneo ya kimataifa; Tatu ni ushirikiano huo unapaswa kushirikisha mataifa yote duniani haswa mataifa yanayoendelea.

Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa UNESCO Irina Bokova, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Shanghai Prof. Li Yansong na viongozi wengine wametoa hotuba katika uzinduzi huo.

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua, Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan na Mwenyekiti wa Shirikisho la Utafiti wa Utamaduni wa Ukonfyusia Duniani Bw. An Lezhe wamezindua Jumuiya ya Utafiti wa Maeneo ya Kimataifa kwa pamoja.

Kongamano la Maendeleo ya Utafiti wa Maeneo ya Kimataifa limefanyika baada ya kumalizika kwa uzinduzi huo.