Mwanzo > Habari > Content

BFSU yaandaa Kongamano la Mageuzi na Maendeleo ya Elimu ya Msingi ya Lugha za Kigeni

Updated: 2022-05-23

Mnamo Mei 13, Kongamano la Mageuzi na Maendeleo ya Elimu ya Msingi ya Lugha za Kigeni lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing(BFSU) na Shirika la Ufundishaji na Utafiti wa Lugha za Kigeni(FLTRP) limezinduliwa.

Mjumbe wa kudumu wa CCPCC Bw. Zhu Yongxin, Mkuu wa Idara ya Elimu ya Msingi ya Wizara ya Elimu Bw. Lv Yugang na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Wang Dinghua wametoa hotuba kwenye kongamano hilo.

Kongamano hilo limehudhuriwa na wakuu wa idara za elimu kutoka kote nchini, walimu wa Kiingereza wa shule mbalimbali, watafiti wanaoshughulikia elimu ya kimataifa, wanachama wa Shirikisho la Elimu la China na kadhalika. Mjadala wa kina umefanyika kwa kuzingatia mada ya “Mageuzi ya Ufundishaji wa Lugha za Kigeni na Maendeleo ya Taaluma za Walimu katika Marekebisho Mapya ya Mitaala”.

Kongamano hilo pia limezindua“Ripoti ya Mwaka ya Utafiti wa Lugha za Kigeni za Msingi” na “Ufumbuzi wa Kidijitali wa Huduma za Elimu”.

14CC9