Kuanzia Mei 27 hadi 28, Kongamano la 2022 la Ushirikiano na Maendeleo ya Kikanda kati ya China, Japani na Korea Kusini lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing (BFSU) limefanyika kwenye mtandao. Kaulimbiu ya kongamano hilo ni "Ushirikiano kati ya China, Japani, Korea Kusini na Asia Mashariki chini ya Ujumuishaji wa Kiuchumi wa Kikanda". Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan na zaidi ya wataalamu na wasomi 60 kutoka vyuo vikuu mbalimbali vya ndani na nje ya nchi wamehudhuria kongamano hilo.
Kongamano hilo limeandaa majukwaa matano yenye mada tofauti. Wataalamu na wasomi kutoka China, Japani na Korea Kusini wamewasilisha uchunguzi wao na kujadiliana kwa kina.