Hivi karibuni, Wizara ya Elimu imetangaza orodha za kozi za hali ya juu katika ngazi ya kitaifa na ngazi ya kimkoa. Kozi 21 za BFSU zikiwemo Kihausa na Kiswahili zimeingia kwenye orodha ya kitaifa huku kozi nyingine 10 zimeingia orodha ya kimkoa ikiwa ni pamoja na Kizulu na Kiamhara. Kozi hizo zitapewa kipaumbele cha kujengwa katika miaka mitatu ijayo.
Hadi sasa, kozi 54 za chuo chetu zimeorodheshwa kama kozi za hali ya juu kwa ngazi ya kitaifa na kozi 18 zimeorodheshwa kama kozi za hali ya juu kwa ngazi ya kimkoa.