Mnamo tarehe 25 Juni, Kongamano la 10 la Tafsiri la Asia-Pasifiki lililoandaliwa na Shirikisho la Kimataifa la Watafsiri(FIT), Chama cha Tafsiri na Ukalimani cha China(TAC) na Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing(BFSU) limefunguliwa.
Mkuu wa TAC Bw. Du Zhanyuan, Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan, Mwenyekiti wa FIT Bw. Alison Rodriguez na Mwenyekiti wa Kitivo cha Tafsiri cha Chuo Kikuu cha Kimataifa Bw.Bart Defrancq wamehudhuria kongamano hilo na kutoa hotuba. Kaulimbiu ya kongamano hilo ni "Ushirikiano katika Ulimwengu wa Tafsiri: Enzi Mpya, Mabadiliko Mapya, Miundo Mipya". Takriban wawakilishi 300 wanaoshughulikia tafsiri kutoka nchi na maeneo 35 duniani kote wameshiriki kongamano hilo.