Mwanzo > Habari > Content

Mahafali ya Mwaka 2022 ya BFSU Yafanyika kwenye Mtandao

Updated: 2022-07-11

Mnamo Juni 29, mahafali ya mwaka 2022 ya Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing yamefanyika kwenye mtandao. Mwaka huu, wanafunzi 2,279 wametunukiwa shahada ya kwanza, wanafunzi 1,201 wametunukiwa shahada ya uzamili na wanafunzi 85 wametunukiwa shahada ya uzamivu. Makamu wa Mwenyekiti wa zamani wa SCLF Bw. Tang Wensheng, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua na Mkuu wa Chuo Kikuu Prof. Yang Dan wamehudhuria mahafali.