Mwanzo > Habari > Content

BFSU yaandaa Kongamano la Ngazi ya Juu la Elimu ya Lugha za Kigeni

Updated: 2022-07-23

Mnamo tarehe 12 Julai, "Kongamano la Ngazi ya Juu la Elimu ya Lugha za Kigeni" lililoandaliwa na Kitivo cha Kiingereza cha BFSU na Shirika la Uchapishaji wa Ufundishaji na Utafiti wa Lugha za Kigeni (FLTRP) limefanyika kwenye mtandao. Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Sun Youzhong amehudhuria ufunguzi na kutoa hotuba.

Prof. Diane Larsen-Freeman wa Chuo Kikuu cha Michigan, Prof. Matthew E. Poehner wa Chuo Kikuu cha Pennsylvania, Prof. Wen Qiufang wa Chuo Kikuu cha BFSU na maprofesa wengine wametoa hotuba zenye mada tofauti na kujadili kwa pamoja maendeleo ya elimu ya lugha za kigeni.