Mwanzo > Habari > Content

Darasa la ukonfusia wa kimataifa na walimu wa utamaduni wa kichina Lafunguliwa

Updated: 2022-08-11

“Darasa la ukonfusia wa kimataifa na walimu wa utamaduni wa kichina la mwaka 2022lililofadhiliwa na Shirikisho la Ukonfusia wa Kimataifa (ICA) pamoja na Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing (BFSU) limefunguliwa tarehe 18 Julai. Naibu mweny wa ICA Bw. Zhang Xuezhi, makamu mkuu wa BFSU Prof. Zhao Gang, wataalamu wa ndani na nje ya China na wanafunzi wa darasa hilo wamehudhuria ufunguzi huo.

Darasa hilo la siku 13 litasomeshwa kwa Kichina na Kiingereza kwenye mtandao. Zaidi ya wanafunzi 160 wa vyuo vikuu mbalimbali kutoka nchi 24 wamejiunga na darasa hilo.