Mwanzo > Habari > Content

Kambi ya Majira ya Joto ya “Uzuri wa Utamaduni” ya BFSU kwa Urusi yafunguliwa

Updated: 2022-08-20

Mnamo tarehe 1 Agosti, Kambi ya Majira ya Joto ya “Uzuri wa Utamaduni” ya BFSU kwa Urusi umefunguliwa kwenye mtandao. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Lugha cha Kitaifa cha Moscow Innara Guseynova, na Makamu Mkuu wa BFSU Prof. Jia Wenjian wamehudhuria ufunguzi huo.

Kambi hiyo inafadhiliwa na Kituo cha Mawasiliano na Ushirikiano wa Lugha cha Wizara ya Elimu, Ofisi ya Taasisi ya Confucius ya BFSU pamoja na Shirika la Uchapishaji wa Ufundishaji na Utafiti wa Lugha za Kigeni (FLTRP). Kambi hiyo ya majira ya joto ya siku 8 inazingatia kujifunza Kichina na utamaduni wa Kichina. Wanafunzi 207 wa zaidi ya vyuo vikuu 60 wanaotoka miji 31 ya Urusi wamejiunga na kambi hiyo.

Katika majira ya joto ya 2022, Ofisi ya Taasisi ya Confucius itaendelea kutumia lugha nyingi za BFSU na kutekeleza programu 10 za mawasiliano ya utamaduni za "Daraja la Kichina". Programu 6 zinawalenga wanafunzi wanaojifunza Kichina kutoka Urusi, Vietnam, Malaysia, nchi na maeneo yanayotumia Kifaransa na nchi za Kiarabu huku programu nyingie 4 zikiwalenga wanafunzi wanaojifunza Kichina duniani kote. Kambi za majira ya joto zinajumuisha mada mbalimbali. Hadi sasa, zaidi ya wanafunzi 1,000 wamejiandikisha kwenye kambi 10 za majira ya joto, na kambi 5 za majira ya joto zimefunguliwa.