Mwanzo > Habari > Content

Kongamano la Wakuu wa Taasisi za Confucius Lafunguliwa

Updated: 2022-09-24

Mnamo tarehe 14 Septemba, Kongamano la Wakuu wa Taasisi za Confucius lililoandaliwa na Wakfu wa Elimu ya Kichina ya Kimataifa (CIEF), Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing (BFSU) na Shirika la Uchapishaji wa Ufundishaji na Utafiti wa Lugha za Kigeni (FLTRP) limefunguliwa kwenye mtandao. Katibu Mkuu wa CIEF Bw. Zhao Lingshan, Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan, Makamu Mkuu wa BFSU Prof. Jia Wenjian wamehudhuria ufunguzi huo.

Kongamano hilo linalenga kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za Confucius, kuimarisha msingi wa maendeleo na kujadili kwa pamoja njia ya maendeleo endelevu ya hali ya juu katika siku za usoni. Kongamano hilo litaendelea hadi Septemba 24, wakuu wa taasisi za Confucius watajadiliana na kupeana maarifa kuhusu mada mbalimbali. Kongamano hilo pia litamwalika Profesa Roger T. Ames kutoka Chuo Kikuu cha Hawaii kueleza uelewa na mawazo yake kuhusu utamaduni wa kikonfusimu.

Kongamano hilo linajumuisha mihadhara 2 maalum na mijadala midogo 3. Karibu wakuu 600 wa ndani na nje ya China wamejiandikisha kushiriki na wakuu 26 watatoa hotuba.