Hivi karibuni, Idara ya Kitaifa ya Utamaduni na Elimu ya nchi za "Ukanda Mmoja na Njia Moja" imechapisha vitabu 20 kwa ujumla ikiwa ni pamoja na "Utafiti wa Utamaduni na Elimu wa India", "Utafiti wa Utamaduni na Elimu wa Iran", "Utafiti wa Utamaduni na Elimu wa Cuba" na "Utafiti wa Utamaduni na Elimu wa Kenya". Maudhui ya vitabu hivi yanajumuisha hali ya kitaifa, mila za kitamaduni, historia ya elimu na fani nyingi nyingine za nchi 20 za “Ukanda Mmoja, Njia Moja” kama vile Kenya, Tanzania, India na kadhalika. Vitabu hivyo vinawawezesha wasomaji kuelewa utamaduni na elimu za nchi hizo na kutoa ushauri na fikra mpya kwa mageuzi na maendeleo ya elimu ya China.