Mnamo 2022, Ofisi ya Kitaifa ya Mipango ya Falsafa na Sayansi ya Kijamii imetangaza kuwa miradi kadhaa ya NSSFC ya BFSU imekamilika kwa ufanisi. Miongoni mwao, miradi mitatu muhimu ambayo imepata tuzo ya “miradi bora” ni mradi uliosimamiwa na Makamu Mkuu wa BFSU Prof. Sun Youzhong, "Ufafanuzi na Utafiti wa Matumizi ya ‘Vigezo vya Kitaifa vya Ubora wa Ufundishaji wa Lugha za Kigeni katika Vyuo Vikuu’, mradi muhimu uliosimamiwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Lugha za Kigeni na Elimu cha China Prof. Wang Wenbin na mradi wa vijana uliosimamiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Kipolish Prof. Li Yinan. Hadi sasa, asilimia ya miradi bora ya NSSFC ya BFSU mwaka huu imefikia 37.5%.