Mwanzo > Habari > Content

Kongamano la Kimataifa la Uenezi wa Utamaduni wa Kichina la 2022 lafunguliwa BFSU

Updated: 2022-11-20

Mnamo tarehe 10 Novemba, 2022, Kongamano la Kimataifa la Uenezi wa Utamaduni wa Kichina la 2022 lililoandaliwa na Kituo cha Uenezi wa Utamaduni cha Shirika la Uchapishaji la Lugha za Kigeni la China, Taasisi ya Uenezi wa Kimataifa wa Utamaduni wa Kichina ya BFSU, na Kituo cha Utafiti wa Ustaarabu wa China limefunguliwa katika BFSU.

Mkuu wa Shirika la Uchapishaji wa Lugha za Kigeni la China Bw. Du Zhanyuan, Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ukonfusia wa Kimataifa Bw. Jia Deyong, na viongozi wengine wamehudhuria kongamano na kutoa hotuba. Takriban wageni 100 wa ndani na nje ya nchi wamefanya majadiliano ya kina.

Kaulimbiu ya kongamano hilo ni “Uenezi wa Kimataifa wa Ustaarabu wa China na Mawasiliano ya Ustaarabu ndani na nje ya China”. Wataalamu na wasomi wanaoshughulikia utafiti wa uenezi wa kimataifa wa utamaduni wa Kichina kutoka nchi mbalimbali wamealikwa kuhudhuria kongamano ili wachunguze thamani ya kisasa na umuhimu wa utamaduni wa Kichina kwa pamoja. Aidha, kongamano hilo lina vikao vinne sambamba ambavyo vinajadili njia za uenezi wa kimataifa wa utamaduni wa Kichina.