Kuanzia tarehe 26 hadi 27 Novemba, Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Utafiti wa Vitabu vya Kiada vya Lugha za Kigeni limefunguliwa kwenye mtandao. Kaulimbiu ya kongamno hilo ni "Utafiti wa Vitabu vya Kiada vya Lugha za Kigeni: "Upeo wa Ulimwengu na Uvumbuzi wa Kienyeji". Takriban wataalamu na wasomi 10,000 wanaoshughulikia elimu ya lugha za kigeni wamehudhuria kongamano hilo. Naibu Mkurugenzi wa Ofisi ya Vitabu vya Kiada ya Wizara ya Elimu, Bw. Chen Mao, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Prof. Wang Dinghua na viongozi wengine wameshiriki kwenye ufunguzi.
Kongamano hilo limekuwa na sehemu tatu ikiwa ni pamoja na ripoti kuu, majadiliano juu ya mada maalumu na hotuba za kikundi. Wataalamu na wasomi wa ndani na nje ya nchi wamejadiliana kwa kina juu ya mada mbalimbali.