Tarehe 8 Desemba, Mkutano wa Kimataifa wa Elimu ya Kichina umefanyika Beijing. Naibu Waziri Mkuu wa China Sun Chunlan amehudhuria ufunguzi na kutoa hotuba. Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan ameshiriki kwenye ufunguzi wa mkutano huo na kutoa hotuba kwenye "Kongamano la Kwanza la Mawasiliano na Ushirikiano kati ya Lugha za Kigeni na Lugha ya Kichina" ambalo ni mojawapo ya makongamano sambamba ya mkutano huo.
Kaulimbiu ya Kongamano la Kwanza la Mawasiliano na Ushirikiano kati ya Lugha za Kigeni na Lugha ya Kichina ni "Kuunganisha, kuwasiliana na kuelewana—Kujenga Uaminifu na Ushirikiano kupitia Lugha na Utamaduni". Mkurugenzi wa Kituo cha Mawasiliano na Ushirikiano wa Lugha ya Kichina na Lugha za Kigeni Bw. Ma Jianfei, Balozi wa UAE nchini China Bw. Ali Zahiri na wageni wengine wamehudhuria ufunguzi wa kongamano na kutoa hotuba. Zaidi ya wataalamu na wasomi mia moja kutoka kote ulimwenguni na wawakilishi wa taasisi mbalimbali za lugha na utamaduni wameshiriki katika kongamano hilo.
Kongamano hilo pia limetoa "Pendekezo la Mawasiliano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Lugha" lililoanzishwa na Kituo cha Mawasiliano na Ushirikiano wa Lugha ya Kichina na Lugha za Kigeni.