Mwanzo > Habari > Content

Kongamano la Jumuiya ya Taaluma ya Nchi na Maeneo ya Kimataifa Lafunguliwa katika BFSU

Updated: 2022-12-30

Tarehe 18 Desemba, Kongamano la Jumuiya ya Taaluma ya Nchi na Maeneo ya Kimataifa la 2022(CCAS) lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing limefanyika kwenye mtandao. Kaulimbiu ya kongamano hilo ni “Ujumuishi, Ushirikiano na Maendeleo Endelevu ya Ulimwengu".

Jumuiya ya Taaluma ya Nchi na Maeneo ya Kimataifa (CCAS) ni mtandao wa kitaaluma ulioanzishwa na Shirikisho la Kimataifa la Vyuo Vikuu vya Lugha za Kigeni (GAFSU), ambao unajumuisha wasomi kutoka nchi 181 wanaoshughulikia zaidi ya lugha 100.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha BFSU Prof. Yang Dan, Mbunge wa zamani wa Morocco Bw. Mohamed Khaliri na Mkuu wa Chama cha Tafsiri na Ukalimani cha China (TAC) Bw. Du Zhanyuan wametoa hotuba kwenye ufunguzi wa kongamano hilo. Wasomi wa ndani na nje ya nchi wamefanya mijadala ya kina kulingana na mada ya kongamano.

Tovuti ya Jumuiya ya Taaluma ya Nchi na Maeneo ya Kimataifa imeanzishwa rasmi kwenye kongamano hilo, dibaji ya kwanza ya “Taaluma ya Nchi na Maeneo--Mtazamo wa Ulimwengu” na kitabu kipya cha "Faharisi ya Dunia ya 2022" pia zimetolewa katika kongamano hilo.